PASS YATEMBELEA KIKUNDI CHA MVUMI GRAPES FARMERS MKOANI DODOMA

Hii ni video fupi ya mwenyekiti wa Mgogoni AMCOS Ltd - Mvumi Mission, iliyopo Wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma akitoa shukrani ya kutembelewa na Mkurugenzi wa biashara wa PASS, Bw. Killo Lusewa alieambatana na meneja wa PASS tawi la Morogoro Bi. Hadija Ngajima, kwa lengo la kutathmini uwezekano wa kuwawezesha kwenye sekta nzima ya kilimo cha Zabibu.

PASS Trust ni taasisi inayowasaidia wakulima na wafugaji kupata mitaji katika benki ili waweze kuwekeza katika shughuli zao za kilimo na ufugaji. PASS inafanya kazi na benki zifuatazo TADB, CRDB, NMB, Bank of Africa (BOA), ACCESS Bank, Post Bank, Equity Bank,Vision Fund Micro-finance Bank, Mkombozi Commercial Bank,Kilimanjaro Co-operative Bank,Bank ABC,Bank M, AMANA Bank, AKIBA Commercial Bank na TIB.

Posted 1 year ago in OTHER